Monday, August 22, 2016

FAIDA YA JUU SANA KATIKA KAZI

Faida ya juu sana aipatayo mtu kwa kufanya kazi sio anachokipata katika kazi hiyo bali ni anachokuwa katika kazi hiyo -John Ruskin

Watu wengi hutenda mambo au hufanya kazi fulani ili apate mapato fulani mfano mafao, pesa nk. Si jambo baya kufanya kazi au kujishughulisha katika mambo fulani kwa mapato fulani lakini sio mtazamo endelevu wa maendeleo. Robert Kiyosaki aliwahi kusema kuwa katika kazi yeyote angalia zaidi hiyo kazi ina manufaa gani zaidi katika kukuongezea maarifa na thamani.

Wekeza zaidi katika kuongeza thamani na hiyo ndiyo iwe faida yako namba moja. Unapojali zaidi thamani inayoongezeka ndani yako unajijengea msingi wa maendeleo endelevu. Thamani ya mtu ni uwezo alionao ndani yake na thamani ya mtu itamuwezesha kuendelea katika mazingira tofauti tofauti.

Unapowekeza katika kuwa na maendeleo ya nafsi mfano mitazamo chanya, maarifa endelevu, uwezo wa kustahimili na tabia za uwajibikaji unajijengea thamani zaidi ya pesa unazopata.
Kama unachofanya kinakuza mfuko wako lakini hakikuzi nafsi yako na kukujenga basi hakikusaidii sana maana pasipo thamani ukija kupoteza hayo mafao ni vigumu kutengeneza mazingira ya kuzalisha.

Thamani yako itakuwezesha kuwa na ufanisi katika eneo lolote. Hivo kwa mujibu wa John Ruskin hiyo ndiyo faida ya juu sana unayoweza kuipata. Hivo badala ya kuangalia zaidi malipo utakayopata angalia zaidi mabadiliko au thamani unayopata au utakayopata katika jambo ulifanyalo.

1 comment: