Monday, August 15, 2016

HUWEZI FANIKIWA ZAIDI YA MAWAZO YAKO

Watu wengi hupenda mafanikio na kukua lakini hawafanikiwi wala kukua. Kwasababu ya sheria moja ambayo ni kwamba huwezi fanikiwa zaidi ya mawazo yako. Maisha yako ya nje ni zao la mawazo yako.

Hakuna jambo linaloweza kutokea kama hujalifikiria kwa wakati wowote katika maisha yako. Unaweza kupenda kufanikiwa lakini je ulishawahi kufikiria na kutafakari mafanikio. Huwezi kuwa na fikra za ukomo halafu uwe na ziada. Mfumo wako wa fikra unadhiirika kwa kauli zako na mitazamo yako juu ya jambo fulani.

Ukishakiri kwamba jambo haliwezekani ni kwasababu umefikiria haliwezekani na halitokuja kuwezekana kwako hadi ubadilishe jinsi unavoliwaza hilo jambo. Hapo pekee ndo utaweza kufungua ubongo wako juu ya njia za kuliweza.

Myles munroe alishawahi kusema ugumu wa jambo fulani unatokana na ufahamu wako juu ya jambo husika hivo badala ya kushikiria mtazamo wako, wekeza kupata ufahamu zaidi juu ya hilo jambo. Huwezi ishi nje ya mitazamo yako maana mitazamo yako siku zote itachonga muundo wa maisha yako.

No comments:

Post a Comment