Moja ya changamoto tunazokumbana nazo katika maisha ni vikwazo vinavotukwamisha kufikia malengo au yale tunayoyahitaji. Kuna vikwazo vya nje na vikwazo vya ndani. Maana halisi ya kikwazo ni jambo linalokuzuia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Vikwazo vinaweza kuwa watu, tabia au hata mifumo ya utendaji. Unapokuwa mtu wa kutafakari maono yako na hapo ulipo utatambua ni aina gani ya kikwazo unachokumbana nacho. Kikwazo siku zote kina namna yake ya kukiangalia ili uweze kukiondoa au kukivuka.
Lazima ujitafakari ni kikwazo cha namna gani unachokumbana nacho na ni nini unaweza kufanya kukivuka hicho kikwazo. Pasipo kukaa chini kujitafakari vikwazo vinaweza kuwa sababu yako ya kulaumu, kulalamika na kujenga mtazamo asi wa maisha.
Njia pekee ya kuvuka kikwazo ni lazima kwanza ujue na uwe na picha halisi ya lengo lako au hatma yako, kisha lazima utulize akili na kisha ukitazame kikwazo kilichopo mbele yako na ukitambue kuwa ni kikwazo cha namna gani.
Kisha ni muhimu sasa kuangalia kikwazo hicho kina mguso gani katika mfumo wako wa kukabili mambo, je hicho kikwazo kinahitaji ufanye mabadiliko gani kwa upande wako, kisha yakupasa uangalie fursa zilizopo za kuweza kukivuka hicho kikwazo.
Kumbuka usipokaa ukatafakari utakuwa unavamia vikwazo na vinakuwa na mguso wa ndani katika nafsi yako kupelekea wewe kukosa kabisa ari na hata morali ya kufanya mambo kupelekea kukata tamaa na kupoteza kabisa mtazamo chanya na maisha.
No comments:
Post a Comment