Thursday, October 13, 2016

SAUTI TATU KATIKA MAHUSIANO

Mahusiano yetu huguswa na sauti ambazo zinaleta changamoto na ni sauti ambazo zinamchango katika uimara wa mahusiano yako au kuanguka kwa mahusiano yako. Bila sauti hizo kuwa katika uwiano  sawa basi sauti moja ikiizidi nyenzake inaweza sababisha changamoto.

Sauti hizo zimegawanyika katika makundi matatu, ya kwanza ni sauti ya nafsi ; Hii ni sauti ambayo kila mtu anakuwa nayo kiasili nayo ni sauti ya uhuru, furaha na amani. Kila nafsi inataka kuwa katika uhusiano ambapo itakuwa huru na yenye furaha na amani, sauti hii inalia kutoka ndani ya nafsi ya mtu na ndio maana kuna ambao husema kuwa katika uhusiano ambao utakuwa huru na mwenye furaha na amani.

Sauti ya pili ni sauti ya Jamii; hii ni sauti inayotoka katika jamii inayotuzunguka juu ya mahusiano yetu. Hii sauti inaweza ikawa sauti ya wazazi au sauti ya malezi na makuzi ambayo tumeyapitia. Sauti hii mara nyingi hutuambia kuwa ni nani anatufaa, au ni nani tunatakiwa tuwe naye au ni mahusiano gani ambayo inabidi tuwe nayo.

Sauti ya tatu ni sauti ya akili zetu; Binadamu huwa na hali ya kupenda kutafakari na kutumia akili katika kufanya maamuzi na pengine kuna wakati hutumia zaidi akili katika mambo fulani juu ya nini hasa jambo sahihi la kufanya.

Ili kujenga uhusiano imara lazima hizi sauti ziwe na uwiano...sauti ya nafsi inabidi iwe kama msingi itakayobeba sauti nyingine zote. Sauti ya nafsi ikizifunika sauti nyingine zote unaweza pelekea kufanya mambo ambayo yanaweza kutokubalika katika jamii na ukajikuta unakosa kabisa ushirikiano na wengine lakini sauti ya jamii ikiizidi sauti ya nafsi utajikuta unaingia katika mahusiano ambayo katika jamii unasifika lakini ndani ya nafsi yako unakosa furaha na unakuwa na upweke ambao jamii haiwezi kukusaidia.

Pia inakupasa sauti ya nafsi iwe na uwiano na sauti ya akili ili akili yako iweze kuwekeza zaidi...maana nafsi na akili zikiwa na uwiano ile amani na furaha hudhiirika katika fikra za ubunifu zaidi katika kuimarisha mahusiano hayo.

Kama unaona sauti ya jamii ni kubwa na inakutisha hakikisha sauti ya nafsi na sauti ya akili vinaungana kuishurutisha sauti ya jamii itulie.

Changamoto na jambo la msingi kwa kila mtu ni kuhakikisha hizo sauti zina uwiano ili kujenga mahusiano imara.


No comments:

Post a Comment