Friday, August 26, 2016

ACHA KUJILINGANISHA NA WATU WENGINE

Moja ya changamoto ambayo huwafanya watu wengi wasiishi katika furaha ni tabia ya kujilinganisha na watu wengine. Washindi hawajipimi kwa maendeleo ya wengine bali kwa maendeleo waliyonayo jana. Bill gates muanzilishi wa Microsoft aliwahi kusema kuwa kujilinganisha na wengine ni kujitukana mwenyewe.

Ukipenda kujilinganisha na watu wengine kuna hatari ya kudharau uwezo wako na kuanza kutazama  madhaifu yako na hii itakujengea tabia ya kutofurahi hata kwa vitu ulivonavo huku ukiwa unatazama zaidi vitu vya wengine au mafanikio ya wengine.

Ukijilinganisha na wengine utaua msukumo wako wa mafanikio kwasababu kuna ambao wamekutangulia katika safari ya maendeleo, kuna ambao wamepitia vikwazo vingi au kuna ambao wamepitia njia rahisi zaidi hivo si busara kujilinganisha na watu.

Weka malengo yako na ujipime kwa malengo yako na siyo malengo ya watu wengine. Kila mtu ana malengo na mitazamo yake na dhana kuu ya maendeleo ni mfumo uliotumika na sio matokeo. Matokeo hayawezi kuwa sawa kama mifumo ni tofauti hivo ukitazama tu matokeo unaweza ingiwa na hasira kwa kutopata matokeo sawa na mwenzako.

Ukipenda kujilinganisha ma wengine utaishi kama kivuli na hautokuwa na utambulisho wako. Wanaoshindwa huangalia zaidi wanaoshinda badala ya kuangalia ushindi. Usiridhike na mafanikio yako ya nyuma...unaweza kuwa zaidi ya hapo.

JE UNAWEZAJE KUJENGA TABIA YA KUTOJILINGANISHA NA WENGINE

1. JITAMBUE : Inakupasa kujitambua wewe ni nani, vipawa vyako, uwezo wako, maarifa yako na yale unayoweza kuyafanya. Jipime kwa hayo mambo na ujiulize Je unaweza kufanya zaidi ya hapo?

2. JENGA MIFUMO: Siku zote husipokuwa na mifumo ya utendaji yako iliyojengwa na mitazamo uliyonayo kuhusu maisha lazima utajaribu kujilinganisha na matokeo yanayopatikana na mifumo inayotumiwa na wengine.

3. EPUKA MANENO YA WATU : Mara nyingi tunajikuta wahanga wa kujilinganisha na wengine kutokana na misukumo tunayoipata kutoka kwa watu wanaotuzunguka kama wazazi, watu wa karibu n.k...Lakini lazima uwe na uwezo wa kutotafakari sana maneno ya watu hasa wale wanaokushinikiza kuwa kama watu wengine.

4. KUMBUKA WEWE NDIO KIONGOZI WA MAISHA YAKO: Inakupasa utambue wewe ni kiongozi wa maisha yako, maisha yako ni kama kampuni hivo yakupasa kujua mtu pekee ambayo ana wajibika zaidi ni wewe. Hata mzazi wako sio kiongozi wa maisha yako zaidi yako wewe. Hii itakusaidia kuwa na mtazamo wa ubunifu zaidi juu ya maisha yako.

5. ANGALIA MBELE : Dereva bora ni yule anayeangalia mbele anapoendesha gari na sio kuangalia pembeni wanaomu overtake au walio ktk mwendo sawa na yeye. Siku zote usitumie muda wako mwingi kutazama wanaoku overtake. Unaweza jifunza jambo lakini si busara kujilinganisha na waƓ

Kumbuka kipimo pekee cha mafanikio yako ni malengo yako na uwezo wako na sio kujilinganisha na wengine.


No comments:

Post a Comment